Ruto alisema katika ujumbe kwenye Twitter kwa Odinga “Kama unavyojua siku zote, nipo tayari kukatana nawe ana kwa ana wakati wowote utakaokufaa.”
Tangu mwezi Machi, muungano wa Odinga wa Azimio umefanya maandamano kwa jumla ya siku tisa dhidi ya serikali, huku maandamano hayo yakibadilika mara kwa mara kuwa uporaji na mapambano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji.
Odinga aliomba maandamano yasitishwe mwezi Aprili na Mei baada ya Ruto kukubali kufanya mazungumzo, lakini mazungumzo hayo yalikwama, huku muungano wa Azimio ukiandaa duru kadhaa za maandamano mwezi huu.
Takriban watu 50 waliuawa katika vurugu tangu mwezi Machi, kulingana na muungano wa Azimio. Lakini takwim rasmi zinasema watu 20 ndio waliuawa.
“Tunashuhudia ukatili uliokithiri wa polisi,” Odinga aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mapema Jumanne katika mji mkuu, Nairobi.
Alisema “ Polisi na magenge yaliyoajiriwa walipiga risasi na kujeruhi watu kadhaa, akiongeza kuwa ghasia hizo zililenga watu kutoka kabila lake la Wajaluo.
Ruto alitetea mwenendo wa polisi, alisema wiki iliyopita “Hatutaki nchi yenye ghasia au mapigano wala uharibifu wa mali.”
Forum