Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:35

Afrika Kusini: Ramaphosa aapishwa kama rais


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Kulia, aapishwa kwenye uwanja wa Loftus Versfeld stadium mjini Pretoria, May 25, 2019.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Kulia, aapishwa kwenye uwanja wa Loftus Versfeld stadium mjini Pretoria, May 25, 2019.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini aliapishwa Jumamosi kwa awamu mpya ya miaka mitano kama kiongozi wa nchi hiyo kwenye hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, na umati wa takriban watu 32,000 kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Pretoria.

Katika Hotuba yake, Ramaphosa, mwenye umri wa miaka 66 alisema kwamba raia nchi hiyo wana matumaini makubwa na kuwashukuru wapiga kura ambao, alisema, walimtunuku hadhi na heshima kuu kwa kumchagua, lakini akaeleza kwamba anafahamu changamoto zilizo mbele yake.

Rais huyo alichukua usukani kwa mara ya kwanza mwaka jana, baada ya raia aliyemtangulia, Jacob Zuma, kulazimishwa kujiuzulu, huku akikabiliwa na shutuma kadhaa za ufisadi, ikiwa ni pamoja na kutumia takriban dola milioni 20 kukarabati nyumba yake binafsi.

Licha ya kuchaguliwa kwa Ramaphosa, ushawishi na umaarufu wa chama kinachotawala cha ANC, umepungua. Kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini, ANC kilipata chaini ya asili mia 60 ya kura.

Kati ya viongozi waliohudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa ni rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais John Magufuli wa Tanzania, Paul Kagame wa Rwanda, Salva Kiir wa Sudan Kusini, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na waziri mkuu wa China, Li Keqiang. Ramaphosa anatararajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri wiki ijayo.

XS
SM
MD
LG