Barua hiyo iliyopelekewa maafisa wa zamani na wa sasa 75 wa serikali hapo Mai 3 2012 na kutangazwa Jumatatu, inatoa msamaha kwa maafisa wa serikali na watu wenye uhusiano na serikali watakao rudisha fedha walozichukua.
Inakisiwa kwamba dola bilioni 4 hazijulikani zilipo au zimeibwa na maafisa wa serikali. Barua hiyo imetolewa wakati Sudan Kusini inatafuta fedha kutokana na kupoteza mapato ya taifa baada ya kusitishwa uzalishaji mafuta.
Hata hivyo wakosowaji wamekua wakiikosoa serikali ya Rais Salva kiir kwa kutopambana na ulaji rushwa loanza kukithiri katika taifa hilo jipya na kuzuia juhudi za kusaidia kujenga taifa hilo lililoharibiwa na vita na lililojinyakulia uhuru kutoka Sudan mwezi wa Julai mwaka jana.
Waziri wa habari wa sudan Kusini Bamaba Marial Benjamin anaema zaidi ya nusu ya fedha hizo zinatokana na kile kinachojulikana nchini humo kama kashfa ya "durra", ambayo inahusiana na mpango wa serikali kununua mtama lakini haukugawiwa wananchi.