Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:09

Rais Kenyatta afanya mabadiliko katika serikali yake


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (R) na Naibu Rais William Ruto.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (R) na Naibu Rais William Ruto.

Maoni na hisia tofauti zimetanda nchini Kenya kuhusu hatua ya Rais Uhuru Kenyatta ya kuteuwa baraza jipya la mawaziri na kuwatimua kazini mawaziri sita wanaotuhumiwa kwa rushwa na wizi wa fedha za serikali. Pia Rais Kenyatta ameongeza baraza lake la mawaziri na kuwateua makatibu wapya wa wizara na mashirika ya umma.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Kenyatta Alitangaza kupitia televishoni ya Taifa mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri na kujaza nafasi za mawaziri hao ambapo sasa ni rasmi kwamba mawaziri hao sita hawatarudi tena kwenye serikali baada ya nafasi zao kuchukuliwa na mawaziri wapya.

Lakini Rais Kenyatta hakuwabadilisha mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni, fedha, ulinzi na usalama wa ndani wote watasalia palepale. Hata hivyo ameongeza idadi ya mawaziri kutoka 19 hadi 20 baadhi yao ni wanawake 4 na wanaume 16. Katika mabadiliko hayo pia aliongezea idara za serikali na mashirika ya umma. Rais Kenyatta alisema shabaha yake ni kuimarisha utendajikazi wa serikali na kukabiliana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kiongozi wa upinzani, Raila odinga
Kiongozi wa upinzani, Raila odinga

Wakati huo huo Muungano wa upinzani unadai mabadiliko hayo hayatoshi, kwa sababu theluthi moja ya mawaziri wangali nje wanahusika na rushwa. Wanadai waziri wa fedha bwana Rotich anastahili kueleza zilipo shilingi bilioni 289 zilizotolewa kama mkopo wa Eurobond na mataifa ya nje. Pia faida ya pesa hizo hazijulikani zilipo. Kinara wa upinzani nchini kenya bwana Raila Odinga ana mashaka juu ya mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri na kudai ni kama kuipiga kiraka serikali .

Katika siku za hivi karibuni serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilikuwa ikikabiliwa na visa vingi vya rushwa na matumizi mabaya ya pesa za umma jambo lililochangia ukosefu wa imani kwa serikali na kuzorota kwa hali ya uchumi na huduma muhimu za jamii.

Waziri wa zamani wa ugatuzi Kenya, Anne Waiguru
Waziri wa zamani wa ugatuzi Kenya, Anne Waiguru

Serikali ya Uingereza hata hivyo imeunga mkono mabadiliko haya ya baraza la mawaziri na kusema yatarejesha imani ya vitega uchumi kutoka nchi za nje pamoja na mataifa ya ulaya. Nchi ya Marekani na Japan imekuwa ikipinga vikali vitendo vya rushwa kwenye serikali ya Kenya. Lakini hadi hivi sasa hakuna waziri au ofisa mkuu wa serikali anayeshutumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa fedha za serikali ameweza kufunguliwa mashtaka kwenye vyombo vya sharia.

XS
SM
MD
LG