Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:10

Rais Joe Biden asaini sheria inayompa mamlaka ya kuharakisha usafirishaji wa vifaa vya kijeshi kwa Ukraine


Rais Joe Biden akisaini kwenye White House sheria inayompa mamlaka mapya ya kusafirisha kwa haraka vifaa vya kijeshi kwenda Ukraine, May 9, 2022. Picha ya AP
Rais Joe Biden akisaini kwenye White House sheria inayompa mamlaka mapya ya kusafirisha kwa haraka vifaa vya kijeshi kwenda Ukraine, May 9, 2022. Picha ya AP

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amesaini sheria inayompa mamlaka mapya ya kuharakisha usafirishaji wa vifaa vya kijeshi na vifaa vingine kwenda Ukraine wakati uvamizi wa Russia unaendelea.

Ikiiga mfano wa sheria ya wakati wa vita vya pili vya dunia ambayo ilizisaidia nchi za Ulaya kupambana na wanazi wa Ujerumani, sheria hii mpya inampa mamlaka kiongozi wa Marekani kufikia makubaliano ya haraka na Ukraine vile vile na nchi za Ulaya mashariki, kuhusu usafirishaji wa vifaa, kuachana na baadhi ya kanuni za Washington zenye urasimu ambao ni mzito.

Sheria hiyo mpya inakuja baada ya Rais wa Russia Vladimir Putin kuyalaumu mataifa ya magharibi kwamba ndiyo yalisababisha Moscow kuivamia Ukraine, akisema Russia ilijibu dhidi ya “tishio kubwa na lisilokubalika karibu na mipaka yake.”

Lakini kiongozi huyo wa Russia hakutangaza mabadiliko yoyote katika operesheni za kijeshi za Moscow wala kutangaza ushindi, akisisitiza kwamba mashambulizi yaliyodumu kwa wiki 10 sasa yataendelea kwenye ngome za Ukraine katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo baada ya Russia kushindwa kumuondoa madarakani Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky au kuuteka mji mkuu Kyiv.

Putin ametoa hotuba hiyo Jana Jumatatu wakati wa guaride la jeshi katika siku ya kumbukumbu ya ushindi wa Umoja wa Soviet dhidi ya Ujerumani katika vita vya pili vya dunia.

XS
SM
MD
LG