Rais Joe Biden siku ya Alhamisi alipendekeza sheria mpya ya kuharakisha mchakato wa madai ya hifadhi kwa wahamiaji maalum katika mpaka wa Marekani na Mexico, lakini mpango huo ulikabiliwa na pingamizi kutoka kwa mawakili wa wahamiaji na wakosoaji.
Agizo hilo linalenga watu walio na rekodi za uhalifu na wale ambao wanaweza kupatikana bila kustahiki hifadhi kwa sababu zingine.
Mabadiliko yaliyopendekezwa yatamruhusu afisa wa Uhamiaji kuamua kama mtu fulani anastahili kupata hifadhi wakati wa uchunguzi wa awali mpakani, badala ya kusubiri miezi au miaka kwa jaji kuamua. Hili lingeathiri kundi dogo la wahamiaji ambao huenda wasingestahili kupata hifadhi hata hivyo.
Forum