Hata hivyo wabunge kutoka chama cha Democratic wenye msimamo wa mrengo wa kushoto na wale wa mrengo wa kulia kutoka chama cha Republican haraka wameelezea upinzani wao Jumapili kuhusu makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wawili.
Akizungumza kutoka Ikulu ya Marekani Jumapili jioni, rais Biden alisema makubaliano hayo ni “habari njema” na kuwasihi wabunge kuupitisha mswaada huo.
“Makubaliano hayo yanazuia mzozo mbaya zaidi, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa letu,” alisema rais Biden.
Akijibu maswali ya wanahabari akiwa White House, rais Biden amesema kwamba spika McCarthy, alifanya amshauriano kwa nia njema, lakini bado kuna swali iwapo kiongozi wa Republican ana uungaji mkono wa kutosha kutoka katika chama chake wa kupitisha makubaliano hayo.
Forum