Vimbunga hivyo vilipiga siku ya Ijumaa na kuharibu majengo na kuua takriban watu 26, akiwemo mmoja katika jimbo la Alabama.
Kaunti za Mississippi zilizojumuishwa katika tangazo hilo ni Carroll, Humphreys, Monroe na Sharkey.
Miji ya Rolling Fork na Silver City iliathiriwa sana na hali hiyo mbaya ya hewa.
Tangazo hilo linatoa fursa ya watu kupatiwa fedha ili kuwasaidia katika mchakato wa kurejea katika hali ya kawaida, fedha hizo zinajumuisha misaada na mikopo.
Waziri wa Usalama wa Ndani Alejandro Mayorkas, na Deanne Criswell mkuu wa Idara ya seriakli kuu ya masuala ya majanga wanasafiri kwenda Mississippi Jumapili kushugulikia hali ya mambo.