Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:48

Rais Biden ahojiwa kuhusu nyaraka za siri


Rais Joe Biden, wa Marekani, amehojiwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi huru kuhusu jinsi alivyoshughulikia nyaraka za siri, ikulu ya Marekani imesema Jumatatu jioni.

Msemaji Ian Sams, alisema katika taarifa yake kwamba mahojiano hayo yalikuwa ya hiari na yalifanyika katika Ikulu ya Marekani, Jumapili na Jumatatu.

Mahojiano hayo yalihitimishwa Jumatatu, Sams alisema. Uchunguzi huo unaongozwa na wakili maalum Robert Hur, ambaye aliteuliwa na mwanasheria mkuu Merrick Garland, kusimamia suala hilo nyeti kisiasa ili kuepusha migongano ya kimaslahi.

Sams alisisitiza kwamba rais Biden, na White House wanashirikiana. Alielekeza maswali kwa idara ya haki.

Forum

XS
SM
MD
LG