Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:12

Serikali mpya ya Rais Azali Comoro yakosolewa


Rais wa Comoro Azali Assoumani
Rais wa Comoro Azali Assoumani

Rais wa visiwa vya Comoros Azali Assoumani ameunda serikali mpya mwezi mmoja baada ya wananchi kuidhinisha katiba mpya inayo mruhusu kubaki madarakani kwa awamu ya pili.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema serikali hiyo yenye mawaziri 12 na mawaziri wa nchi watatu, haina tofauti na serikali iliyokuwepo awali.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa Rais Azali amefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumuondowa mhasimu wake mkubwa makamu wa Rais Djaffar Said Ahmed aliyepinga mabadiliko ya katiba akisema yanakwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:33 0:00

Sura za zamani

Mohamed Mshangama mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Moroni anasema hakuna watu wapya walochaguliwa katika serikali hiyo.

“Hakuna mabadiliko mapya ya watu, wala serikali hiyo haionyeshi ni njia gani rais anataka kufuata kisiasa. Kwani watu ni wale wale.”

Na zaidi ya hayo Mshangama anasema wale baadhi ya viongozi wa upinzani walio msaidia Azali katika kampeni za kura ya maoni hawakuteuliwa kama ilivyo tarajiwa.

“viongozi wa vyama mbali mbali waliomsaidia Azali katika kura ya maoni hakuna hata mmoja kati yao aliyechaguliwa. Kwa hivyo inaonesha kwamba yeye kawachukua wale watu wake anaowaamini mpaka sasa”.

Kutekelezwa kwa Katiba mpya

Kwa kuwa katiba mpya inatekelezwa ambayo inaleta mabadiliko ya mfumo wa serikali, uchaguzi unahitajika kufanyika katika muda wa siku 90, baada ya kuidhinishwa na wachambuzi wanasema haijulikani lini uchaguzi huo utafanyika.

“Ndio hatujui lini, inasemekana katika muda wa miezi sita ijayo, wengine wakisema utafanyika kati ya Novemba na Disemba wengine mapema mwaka 2018. Kwa vyovyote vile uchaguzi wa rais unabidi kufanyika.”

Na katika habari nyingie za kisiasa imeripotiwa kwamba Rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi aliyewekwa kizuizini nyumbani kwake, kutokana na tuhuma za rushwa na kuuza poaspoti ya nchi kwa Kuwaiti na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Rais wa zamani agoma kula

Azali ameripotiwa kuwa ameanza mgomo wa kula chakula akilalamika dhidi ya hali ya kifungo chake. Mohamed MShangama anasema hawana uthibitisho wa habari hizo zilizoanza kuenea Jumanne.

“Tumeanza kusikia habari hizo tangu jana lakini bado hatujapata uhakika kwamba ameanza mgomo huo. Lakini kama mnavyo fahamu yuko katika kizuizi ambacho ni sawa na jela na ameondolewa mpishi na kuchukuliwa simu zake na tangu jana tumesikia hali chakula isipokua maji”, amesema Mchangama.

Sambi amekanusha kufanya kosa lolote katika kashfa ya passpoti lakini washirika wake wa Kuwait na UAE wamekaa kimya kuhusiana na sakata hilo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG