Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:45

Magufuli amfukuza kazi waziri Muhongo


Rais wa Tanzania John Magufuli
Rais wa Tanzania John Magufuli

Rais John Magufuli wa Tanzania amemfukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo baada ya kupokea ripoti ya tume ya chunguzi wa madini katika makontena 277 .

kamati ya kuchunguza na kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena 277 yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa kwenye maeneo mbalimbali nchini imewasilisha ripoti yake jumatano kwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kuonesha kuwa taifa lingepoteza mapato ya fedha kati ya shilingi bilioni 829.4 hadi trilioni 1.4 kutoka kwenye makontena hayo ambayo yalikuwa yakisubiriwa kusafirishwa nje ya nchi.

utaratibu huo wa kusafirisha makontena ya mchanga wa dhahabu umekuwa ukifanyika kwa takriban miaka 19 iliyopita, na kwa mujibu wa kamati hiyo uchunguzi wao umebaini licha ya dhahabu pekee pia kuna aina zaidi ya nne za madini mkakati ambayo yamebainika kuwa na thamani kati ya shilingi bilioni 108 hadi 231 ambayo hayakufanyiwa ukokotowaji wa mrabaha wa serikali.

kufuatia ripoti hiyo rais Magufuli amechukua hatua kadhaa ikiwemo kumfukuza kazi waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo na ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinashiriki ipasavyo katika ulinzi wa rasilimali za taifa.

Wakati huo huo Magufuli amevunja Bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania TMAA na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

Ripoti iliyowasililishwa katika ikulu ya Tanzania, iliwasilishwa na kamati ya wataalam wa sekta ya madini kubaini aina na kiwango cha madini yaliyo ndani ya mchanga unaosafirishwa kwenda nje.

Katika makontena zaidi ya 200 yaliyokuwa yakichunguzwa, imebainika kuwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja za Tanzania.

XS
SM
MD
LG