Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:46

Raia wa Taiwan wana wasiwasi wa kuvamia na China


Mivutano ikiwa  inaendelea baina ya China, na Taiwan, watu mjini Taipei huwa wanaandmana kutokana na tishio la kushambuliwa na China.

Taiwan imekuwa haina maelewano na chama cha Kimomunisti cha China toka miaka ya 1940, na kwa miongono kadhaa, mivutano inazidi kuongezeka kutokana na jeshi la China kuzidi kuwa la kisasa.

China bado inaichukulia Taiwan ambayo imejitangazia mamlaka yake kuwa ni jimbo lake.

Hali hiyo imejitokeza mara mbili mwaka jana na hasa baada ya Russia kuivamia Ukraine, ambapo hofu kubwa imetanda iwapo uvamizi wa China kwa Taiwan unaweza kufuata.

Mwezi Agosti mwaka jana, Beijing ilifanya mazoezi ya kijeshi na kurusha makombora kwenda himaya ya Taiwan baada ya ziara ya spika wa wakati huo wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi.

XS
SM
MD
LG