Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:03

Raia wa Burundi mfanyakazi wa kampuni ya Boeing, apata tuzo ya muhandisi mweusi bora mwaka wa 2023


Ndege ya Boeing aina 787-9
Ndege ya Boeing aina 787-9

George Ndayizeye, raia wa Burundi anayefanya kazi kwenye kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing yenye makao yake mjini Seattle hapa Marekani, alipata tuzo ya muhandisi bora mweusi mwaka wa 2023, kutokana na mchango wake wa kiufundi kwenye kampuni hiyo.

Mapema wiki hii, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Boeing Stanley Deal aliandika kwenye Facebook “Hongera George Ndayizeye kwa kupata tuzo ya Walt W. Braithwaite Legacy Award” kwa mchango wako mkubwa wa kiufundi.

Ndayizeye mwenye umri wa miaka 41, mzawa wa mkoa wa kusini mwa Burundi wa Makamba, ni muhandisi kwenye kampuni ya Boeing, anayehusika na kuchunguza namna ndege zinavyotengenezwa.

Akizungumza na Idhaa ya Kirundi na Kinyarwanda ya Sauti ya Amerika Jumatano, alisema ‘nilipokea kwa fura kubwa tuzo hiyo.’

“Nilipata tuzo hiyo kutokana na ubunifu mpya na mchango mkubwa wa kiufundi kwenye utengenezaji wa ndege”, alisema.

Ndayizeye amesema alichangia katika utengenezaji wa ndege aina ya Boeing 787 na Boeing 777-9 na ndege nyingine itakayombeba Rais wa Marekani.

XS
SM
MD
LG