Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:07

Raia nane wafariki dunia katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha afya mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwa Kilimanyoka, Kivu Kaskazini, Juni 9 2022. Picha na REUTERS/Djaffar Sabiti
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwa Kilimanyoka, Kivu Kaskazini, Juni 9 2022. Picha na REUTERS/Djaffar Sabiti

Takriban raia wanane walifariki dunia  Alhamisi katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha afya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vilivyowanukuu wenyeji.

Shambulio hilo lilitokea katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo. Wenyeji walisema shambulio hilo lilitokana na wanamgambo wa Allied Democratic Forces, ambao waliahidi uaminifu kwa kundi la Islamic State mwaka 2019.

Kwa sasa tuna idadi ya waliofariki dunia, ikiwa ni pamoja na wagonjwa na mhasibu katika kituo cha afya, kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo la Beni Omar Kalisia aliwaambia waandishi wa habari. Kalisia aliongeza kuwa muuguzi mmoja hakuwepo, na nyumba moja ilichomwa moto.

Shambulio hilo la Alhamisi kwenye kituo hicho cha afya linafuatia shambulio la Mei 3 kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo hilo hilo, na shambulio la Mei 7 katika kijiji kimoja katika jimbo jirani.

Mwishoni mwa 2021, DRC na nchi jirani ya Uganda zilianzisha operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya Allied Democratic Forces. Hadi sasa, jitihada hizo hazijafanikiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG