Lakini ni jina geni miongoni mwa watanzania wengi, na ameanza kusikika hivi karibuni alipojitokeza kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.
Queen mwenye umri wa miaka 67 mzaliwa wa Kijiji cha Rondo mkoani Lindi ni mtaalamu wa biashara na pia anajishughulisha na kilimo na ujasiriamali, alianza harakati za siasa kwenye chama tawala cha CCM, hakuwa na nafasi yeyote ya uongozi katika chama. Mwaka 2014 aliamua kukihama CCM na kuingia ADC ambako jina lake lilianza kupata umaarufu pale mwaka 2015 alipowania ubunge katika jimbo la Kawe. Hakufanikiwa kushinda ubunge ambapo jimbo la Kawe lilichukuliwa na Halima Mdee ambaye aliwania ubunge kwa tiketi ya chama cha Chadema.
Mwaka 2015 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa chama cha ADC kushiriki katika uchaguzi wa vyama vingi.
Wanawake wanasiasa ni kundi dogo kwa wale ambao wanawania nafasi ya juu ya uongozi katika nchi. Mwaka huu tunashuhudia wanawake wawili tu ndiyo wameamua kuoglelea katika maji ya kina kirefu. Nao ni Queen na kwa tiketi ya ADC na Cecilia Augustino Mwanga kwa tiekti ya Demokrasia Makini.
Queen anaingia katika ushindani wa urais akiinadi ilani kuu ya chama chake katika mambo makuu matatu ambayo ni elimu, afya na kilimo.
Queen : “Nafasi ya mwanamke kwenye kuongoza ni nafasi kubwa zaidi, kwasababu kina mama wengi wana sifa uongozi ambao ni wa kiuadilifu. Wana sifa ya uongozi ambao hauna makando kando. Na mimi ni mama na Tanzania tangu ipate uhuru haijapata kuongozwa na kiongozi mkubwa sana wan chi wa jinsia ya kike.”
Mgombea anaelezea mbali na kutaka kuhakikisha watazania wanakuwa katika nafasi nzuri ya kutimiziwa mambo muhimu ya elimu, afya na kilimo lakini pia kuna masuala mengine ambayo waayapa kila umbele katika maisha yao ya kawaida ya kila siku.
Anasema msukumo wake umepata nguvu kwa kuwa ni muumini mkubwa wa maendeleo ya jamii, na hivyo ameona wakati umefika kuwania uongozi ili kusaidiana na wananchi kuleta picha mpya ya kimaendeleo katika taifa.
Wanaharakati na baadhi ya watetezi wa haki za wanawake wanaamini kuwa nafasi ya mwanamke katika uongozi ni kubwa na hasa ikizingatiwa kuwa wanawake wengi wana sifa za uongozi bora.
Mwanahabari mkongwe na mwanaharakati wa masuala ya wanawake, Leila Sheikh anelezea umuhimu wa kina mama kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi, anasema wakati ndiyo huu.
Leila : “Kama wako wanawake, kama mwaka 2015 alijitokeza Mama Anna Mghwira akagombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo. Na kwa kweli alikuwa jasiri. Na alikuwa jasiri alifanya kampeni yake na kampeni yake ilikuwa nzuri. Sioni kama kuna ubaya wowote kama mtu anahisi anaweza kugombea sio mbaya. Na sisi tupo kuwashangilia.”
Kinyang’anyiro cha urais kina wagombea ambao ni wakongwe katika siasa na wanafahamu vyama miki miku ya harakati za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu. Kwa Queen hizi ni changamoto zenye tija zinaongeza hamasa yake kuwepo katika uwanja wa siasa na kulenga katika kumuelimisha mpiga kura kuwa wakati kwa wanawake kushika hatamu za. Uongozi umefika na yeye ni chachu ya maendeleo.
Queen ana Imani kuwa yeye na wanawake wengine wanasiasa wamefungua njia ya maendeleo kwa baadhi ya wanawake wenzao ambao mpaka katika miezi ya karibuni walikuwa hawajafikiria kwa dhati kuwania nafasi za uongozi.
Queen : “Tunategemea wa kina mama wengi wanapopata nafasi ya kuingia kwenye nafasi mbali mbali za uongozi na uamuzi basi watakuwa ni chachu. Lakini pia watakenda kutengeneza usawa wa kijinsia kuhakikisha kwamba mwanamke nab inti wa kitanzania anapata maendeleo na manufaa ambayo ni haki yake bila ya kujali jinsia yake.”
Mgombea urais anaamini ilani ya uchaguzi ya chama chake ya mwaka 2020 mpaka 2025 ni njema, nzuri, ambayo itakuwa na faida kubwa sana kwa Tanzania na pia itakuwa imebeba usawa mkubwa zaidi wa kijinsia kwa mama nab inti wa kitanzania.