Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 03:30

Maandamano dhidi ya ushindi wa Trump yanaendelea


Waandamanaji wapinga baadhi ya sera za Donald Trump.
Waandamanaji wapinga baadhi ya sera za Donald Trump.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, siku ya Jumamosi aliambia kipindi cha Televisheni cha "60 Minutes" kuwa hatafutilia mbali vipengele vya mfumo wa afya wa Obamacare, ambao, kwenye kampeni zake, amekuwa akiwaahidi wafuasi wake kwamba angeubadilisha kabisa.

Kuchaguliwa kwa mfanyabiashara tajiri, Donald Trump, kama rais wa Marekani siku ya Jumanne, kumeendelea kuzua hisia za kila aina, siyo tu baina ya Wamarekani, bali pia raia wa nchi zingine.

Rais huyo mteule tayari ameanza kuiweka pamoja timu itakayosimamia upokezanaji wa mamlaka.

Wakati huo huo, maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi Marekani, na ambao wanapinga sera zake, wliendelea na maandamano kwenye barabara za miji mikubwa nchini humo, kwa siku ya nne mfululizo. BMJ Muriithi anaarifu zaidi..

Maandamano ya kupinga sera za Trump yaendelea
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:49 0:00

XS
SM
MD
LG