Amesema hiyo ni hatua ya mwanzo katika mazungumzo zaidi yatakayofanyika Alhamisi juu ya uwezekano wa kufanyika mkutano mwezi Juni kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump.
Pompeo alituma picha kupitia tweet Jumatano usiku akionyesha akipeana mkono na Kim Yong Chol na picha nyengine ikimwonesha mtu huyo amekaa karibu na meza katika nyumba iliyoko karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.
Alisema pia chakula cha usiku kilikuwa na nyama, mahindi na jibini.
Alhamisi asubuhi, Pompeo amesema kupitia Twitter kuwa “uwezekano wa kuwepo mkutano” kati ya viongozi wanaowakilisha Marekani na Korea Kaskazini inawapa Korea Kaskazini “fursa muhimu ya kufikia usalama na mafanikio ya kiuchumi.”