Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 30, 2024 Local time: 06:49

Polisi wa Uingereza wamkamata mshukiwa wa mauaji ya familia ya mwanahabari wa BBC


Polisi wa Uingereza
Polisi wa Uingereza

Polisi wa Uingereza Jumatano wamempata mtu anayeshukiwa kumuua mke wa mtangazaji wa BBC, John Hunt na binti zake wawili karibu na Enfield kaskazini mwa London. 

Mshukiwa huyo anayetambulika kwa jina la Kyle Clifford mwenye umri wa miaka 26, alikutwa na majeraha na anapewa matibabu, polisi wamesema na kuongeza kuwa hawajui alijeruhiwa vipi lakini hawakufyatua risasi.

Waathiriwa walitambuliwa na BBC kuwa ni Carol Hunt, 61, mke wa John Hunt, na binti zao, wenye umri wa miaka 25 na 28.

Mamlaka za eneo hilo ziliitikia mwito katika makazi ya Bushey, ambapo wanawake hao walipatikana wakiwa wamefariki dunia Jumanne jioni.

Mapema Jumatano, polisi wa Hertfordshire walimtambua Clifford kama mshukiwa, ingawa polisi hawakuthibitisha kama alikuwa na marehemu hao.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeeleza alikuwa mpenzi wa zamani wa mmoja wa mabinti hao.

Forum

XS
SM
MD
LG