Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:05

Kenya: Polisi washutumiwa kuwaua watu 15 kiholela


Mtu ajisalimisha kwa polisi wa Kenya.
Mtu ajisalimisha kwa polisi wa Kenya.

Mamlaka inayoangazia utendakazi wa polisi nchini Kenya IPOA, Jumatano ilisema kwamba Wakenya wapatao 15 wameuawa na polisi katika taifa hilo la Afrika Mashariki katika kipindi hiki ambacho kumewekwa marufuku ya kutoka nje usiku, kati ya masharti mengine, kama hatua za kudhibiti kasi ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mjini Nairobi na mamlaka hiyo, maafisa sita wa polisi watashtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyanyasaji, baadhi wakituhumiwa kuhusika kwa vitendo vya kufyatua risasi kiholela dhidi ya raia wakati wakitekeleza masharti ya marufuku hiyo.

Polisi pia wanatuhumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi badala ya kutii sheria wakati wakitekeleza majukumu yao.

Nalo shirika la umoja wa mataifa la kutetea haki za binadamu, pia linawashutumu polisi wa Kenya kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauaji na unyanayasaji wa kingono kwa baadhi ya raia.

Hata hivyo, idara ya polisi imesema matukio yatanayotajwa katika ripoti hizo, yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina.

Tangu masharti mbalimbali kuwekwa na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo wa Corona, Wakenya katika miji mbalimbali wamekuwa wakilalamikia hulka ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi, na kuwanyanyasa kwa njia mbalimbali.

XS
SM
MD
LG