Wizara ya sheria ya Marekani kitengo cha haki za kiraia kitaongoza uchunguzi kutokana na mauaji yaliofanywa na Polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi nje ya duka la vyakula Jumanne katika jimbo la Luoisiana.
Gavana John Bel Edwards amesema wizara ya sheria itasaidiwa na idara ya maksoa ya jinai FBI katika uchunguzi wake na polisi katika eneo hilo.
Edwards alisema jumatano “nina wasi wasi mkubwa”Video hii inasikitisha sana.
Video hiyo ilionyesha mmoja wa polisi hao akimpiga risasi Alton Sterling mwenye umri wa miaka 37 wakati akiwa amebanwa ardhini. Video hiyo ilipelekea wito wa kujiuzulu kwa mkuu wa Polisi wa mji huo Carl Dabadie.