Maafisa wa ulinzi wa Marekani, Jumatatu walikataa kuthibitisha ripoti za vyombo vya habari kwamba Rais Joe Biden wa Marekani, ameamua kuruhusu Kyiv kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotolewa na Washington kushambulia ndani ya Russia.
Msemaji wa Pentagon, Sabrina Singh, ameiambia VOA kwamba kinacho ongeza mgogoro huo ni ukweli kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini kwa sasa wanapigana Ukraine, kusaidia Moscow.
Marekani, inakadiria kwamba kuna wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wameelekea eneo la Kursk, mkoa unaopatikana kusini mwa Russia, ambao Ukraine, uliushikilia baada ya shambulizi la ghafla mwezi Agosti, na bado inaushikilia.
Forum