Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:08

Marekani yapeleka vifaa zaidi vya kijeshi Saudi Arabia


Waziri wa ulinzi Marekani, Mark Esper akizungumza na waandishi wa habari huko Pentagon hivi karibuni
Waziri wa ulinzi Marekani, Mark Esper akizungumza na waandishi wa habari huko Pentagon hivi karibuni

Msaada huo ni hatua ya kwanza katika kujibu kile maafisa wa Marekani wanachokiita shambulizi la Iran lililofanywa mwanzoni mwa mwezi huu kwenye vinu vya mafuta vya Saudi Arabia

Pentagon inapeleka Saudi Arabia betri za makombora aina ya Patriot, mifumo minne ya rada na kiasi cha wanajeshi 200 ili kusaidia kulinda anga ya nchi hiyo ya kifalme dhidi ya mashambulizi zaidi.

Msemaji mkuu wa Pentagon, Jonathan Hoffman alisema Alhamis upelekaji huo utaongeza nguvu ya ulinzi wa makombora ya anga kwenye miundo mbinu muhimu ya kijeshi na kiraia nchini humo. Hoffman aliongeza kuwa betri mbili zaidi za patriot na mfumo wa ulinzi wa teknolojia ya juu-THAAD pia unaandaliwa kupelekwa huko ili kujikinga dhidi ya makombora kama ikihitajika.

Msaada huo ni hatua ya kwanza katika kujibu kile maafisa wanachokiita shambulizi la Iran lililofanywa mwanzoni mwa mwezi huu kwenye vinu vya mafuta vya Saudi Arabia.

Ofisa mmoja wa Marekani aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba shambulizi lilianzia huko kusini magharibi ya Iran na kwamba Marekani ina ushahidi zaidi wa kuunga mkono madai yake, sio tu mabaki, japokuwa hakuna ushahidi wowote uliotolewa na Marekani hadi hivi sasa.

XS
SM
MD
LG