Rais Donald Trump alikuwepo wakati wa hafla ya kuapishwa kwa mkurugenzi huyo kwenye makao makuu ya CIA nje ya mji wa Washington.
Trump amesema kuwa mwanamke huyo ni “mtu maalum sana… ambaye ametumikia nchi hii kwa kipaji na moyo wa kipekee.”
Amesema kuwa “ hakuna mtu yoyote katika nchi hiii aliyekuwa anastahili zaidi kuchukua wadhifa huu maalum kuliko wewe.”
Baraza la Seneti la Marekani lilimthibisha Haspel Alhamisi iliyopita kwa kura 54 dhidi ya 45, na kumaliza mvutano juu ya mchakato wa kupendekezwa kwake ambapo wabunge walikuwa wamedurusu matukio ya uchunguzi uliofanywa na CIA huko nyuma.
Wademokrati sita walipiga kura kumuunga mkono Haspel, wakati Warepublikan wawili walipinga uteuzi wake ili kuchukua nafasi ya Mike Pompeo, ambaye alithibitishwa Aprili kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.
Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnel, Mrepublikan wa Jimbo la Kentucky, alimpongeza Haspel, Mfanyakazi wa muda mrefu wa CIA, kuwa ni mwenye sifa ya kipekee kuweza kukabiliana na changamoto kubwa za kiusalama za kitaifa,” akiongeza kuwa mwanamke huyo “ameweza kupata heshima na kukubalika na wanaume na wanawake wanaofanya kazi katika CIA.”