Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:20

Papa Wemba afariki akiwatumbuiza mashabiki


Papa Wemba enzi ya uhai wake.
Papa Wemba enzi ya uhai wake.

Papa Wemba mmoja wa wanamuziki mashuhuri sana barani Afrika na anayejulikana duniani kote kama mfalme wa Rumba wa Congo amefariki Jumapili asubuhi baada ya kuanguka kwenye jukwaa nchini Ivory Coast maafisa wamesema. Alikuwa na umri wa miaka 66.

Papa Wemba alifanya maonyesho matatu katika tamasha la Urban Musical Festival Anoumabo (FEMUA) mjini Abidjan kabla ya kuanguka mbele ya maelfu ya washabiki.

Wenzake ambao alikuwa akifanya onyesho pamoja nao waliharakisha kumsaidia, lakini alifariki kabla ya kufika hospitali, maafisa wamesema. Sababu ya kifo haijajulikana.

Alizaliwa Juni mwaka 1949 na kupewa jina la Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba katika iliyokuwa Congo ya Ubelgij. Mwanamuzi huyu amekuwa akifanya maonyesho ya muziki wa kiafrika kwa zaidi ya miongo minne.

Alipanda na kupata umashuhuri mkubwa mwishoni mwa miaka 1960 na mwanzoni mwa 1970 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mji Kinshasa akiwa na bendi yake Zaiko Langa Langa.

XS
SM
MD
LG