Papa Francis kwa maneno ambayo yalionekana kuilenga China badala ya nchi jirani aliyokuwa akiitembelea alisema Jumamosi kwamba serikali hazina chochote cha kuogopa kutoka katika Kanisa Katoliki kwa sababu halina ajenda ya kisiasa.
Francis mwenye umri wa miaka 86, alitoa maoni yake huko Mongolia, nchi ambayo ina Wakatoliki 1,450 pekee na ambapo Kanisa hilo ni dogo nchini humo na lina uhusiano mzuri na serikali ambayo imeonyesha kuthamini shughuli zake za kijamii, afya na hisani.
Katika siku yake ya kwanza nchini Mongolia, serikali ya nchi hiyo ilimpa heshima Papa kwa hafla za kitamaduni kwa gwaride likijumuisha wanaume waliopanda farasi waliovalia kama mashujaa wa zamani wa Mongolia.
Katika hotuba yake kwa maaskofu, mapadre, wamishionari na wachungaji alisema Yesu hakutoa mamlaka ya kisiasa kwa mitume wake bali aliwaambia wapunguze mateso ya binadamu waliojeruhiwa kwa imani.
Forum