Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:29

Papa Francis aelekea DRC lakini hatafika Goma


Papa Francis, akiambatana na msemaji wa Vatican Mchungaji Federico Lombardi, alipowasalimia waandishi wa habari ndani ya ndege kuelekea Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 25, 2015. AP
Papa Francis, akiambatana na msemaji wa Vatican Mchungaji Federico Lombardi, alipowasalimia waandishi wa habari ndani ya ndege kuelekea Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 25, 2015. AP

Papa Francis yuko safarini kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne kwa ziara ambayo itaangazia maadhila yanayowapata binadamu kutokana na  migogoro ya muda mrefu na unyonyaji wa utajiri wa madini wa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati.

Papa huyo mwenye umri wa miaka 86 anatarajiwa kutua katika mji mkuu Kinshasa karibu saa tisa saa za alasiri Jumanne. Baada ya hafla ya kukaribisha na kukutana na Rais Felix Tshisekedi, atatoa hotuba kwa maafisa, wanadiplomasia na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

Siku ya Jumatano, ataongoza Misa na kukutana na wahanga wa ghasia kutoka eneo la mashariki mwa nchi, ambalo limekumbwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya waasi wa kundi la M23 na wanajeshi wa serikali.

Papa aliwaambia waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege yake, kwamba alitaka kwenda Goma lakini hataweza kwa sababu ya vita vinavyoendelea.

Wakati ndege yake ilipokuwa ikipaa juu ya jangwa la Sahara, papa alichukua fursa hiyo kuzungumza kuhusu masaibu ya wahamiaji wa Kiafrika wanaovuka jangwa hilo katika jaribio la kufika Ulaya.

Alsema "Hebu tusimame kwa muda mfupi tukiwa kimya, kuwafikiria na kuwaombea , watu wote ambao, hawakufanikiwa wakiwa wanapita njia hii wakitafuta ustawi bora, uhuru kidogo.

XS
SM
MD
LG