Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 03:13

Pakistan yapinga azimio la bunge la Marekani kuhusu uchaguzi


Pakistan Jumatano imepinga vikali azimio la bunge la Marekani linalotaka uchunguzi ufanyike kuhusu kuingiliwa na madai ya udanganyifu kuhusiana na uchaguzi wa bunge wa Februari 8 nchini Pakistan.

“Tunaamini kuwa muda na muktadha wa azimio hili hauwiani vyema na mienendo chanya ya uhusiano wetu wa nchi mbili,” imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, mjini Islamabad.

Taarifa hiyo imesema azimio hilo linatokana na uelewa usio kamili wa hali ya kisiasa na mchakato wa uchaguzi nchini Pakistan.

Shauri hili la karipio limetolewa siku moja baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kupiga kura kwa wingi 368 za ndio na 7 za hapana Jumanne kuidhinisha azimio linalotaka uchunguzi kamili na huru wa madai ya kuingiliwa au kukiukwa kwa taratibu katika uchaguzi wa Pakistan.

Forum

XS
SM
MD
LG