Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 19:59

Pakistan yakasirishwa na Ujerumani kushindwa kulinda ubalozi wake


Pakistan imelaani Ujerumani kwa kushindwa kulinda ubalozi wake mdogo mjini Frankfurt dhidi ya uvamizi na kuharibiwa Jumamosi na waandamanaji wanaoripotiwa kubeba bendera ya taifa la Afghanistan.

Katika taarifa ya Jumapili iliyotolewa mjini Islamabad, wizara ya mambo ya nje, bila kutaja utaifa wowote maalum, iliwataja washambuliaji hao kama genge la watu wenye itikadi kali na kukemea ukiukaji wa usalama katika ujumbe wa kibalozi, ikisema unahatarisha maisha ya wafanyikazi wake.

“Tunawasilisha maandamano yetu makali kwa serikali ya Ujerumani,” wizara hiyo imesema. Iliitaka Ujerumani kuchukua hatua za haraka ili kutimiza wajibu wake chini ya mkataba wa Vienna wa mahusiano ya kibalozi ili kuhakikisha usalama wa ujumbe wa kidiplomasia wa Pakistani na wafanyakazi nchini humo.

Video ya mitandaoni ya tukio la Jumamosi inaonyesha watu wengi wakiwa wameshikilia viashiria vya raia wa Afghanistan.

Forum

XS
SM
MD
LG