Upinzani ulisusia uchaguzi huo ukisema uliandaliwa bila kuzingatia sheria.
Wanasiasa wakuu wa upinzani wanakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kususia uchaguzi wa Oktoba 31 na kuunda serikali yao.
Ouattara amesema kwamba yupo tayari kwa mazungumzo na wanasiasa wa upinzani ili kutuliza joto la siasa katika nchi hiyo ambayo inazalisha kiwango kikubwa cha kakau duniani.
“Ningependa kusisitiza kwmaba nipo tayari kwa mazungumzo ya wazi na kweli yanayozingatia sheria.” Amesema Outtara katika hotuba kwa taifa.
Amemwalika aliyekuwa rais Hneri Bedie kwa mkutano katika siku za hivi karibuni.
Bedie alijiunga na wanasiasaa wa upinzani katika kususia uchaguzi huo, Pamoja na kuunda serikali mbadala.
Makundi ya upinzani yamesema kwamba Ouattara alikiuka katiba kwa kuwania mhula wa pili madarakani.
Ouattara amesisitiza kwamba katiba mpya ya mwaka 2016 inamruhusu kuanza awamu mpya ya utawala bila kuzingatia mihula miwili aliyotawala.
Ghasia zimetokeoa Ivory Coast kuelekea uchaguzi huo na hata siku ya uchaguzi.
Watu 35 wameuawa katika machafuko hayo ya ghasia.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC