Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 03:23

Olaf Scholz wa Ujerumani ateua baraza la mawaziri la kwanza lenya usawa wa kijinsia


Olaf Scholz wa chama cha Social Democratic Party (SPD) cha Ujerumani
Olaf Scholz wa chama cha Social Democratic Party (SPD) cha Ujerumani

Usawa ni muhimu kwangu na ndio maana kati ya mawaziri 16 kutakuwa na wanaume wanane na wanawake wanane alisema Scholz ambaye anajieleza mwenyewe kama mtetezi wa haki za wanawake

Olaf Scholz ambaye anatarajiwa kuchaguliwa wiki hii kumrithi Angela Merkel kama kansela wa Ujerumani leo Jumatatu aliteua baraza la mawaziri la kwanza lenye usawa wa kijinsia nchini humo huku wanawake wakichukua nyadhifa muhimu za usalama.

Scholz wa chama cha Social Democrat (SPD) alielezea safu ya chama chake kwa serikali ya kwanza inayoongozwa na mrengo wa kati, katika muda wa miaka 16 huku mtaalam anayezungumzia majanga Karl Lauterbach akitajwa kama waziri wa afya.

"Usawa ni muhimu kwangu na ndio maana kati ya mawaziri 16 kutakuwa na wanaume wanane na wanawake wanane alisema Scholz ambaye anajieleza mwenyewe kama mtetezi wa haki za wanawake".

Baada ya chama cha Greens, washirika katika serikali ya mseto ijayo kumtaja kiongozi mwenza Annalena Baerbock kama waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani. Christine Lambrecht wa chama cha SPD hadi sasa ni waziri wa sheria atachukua nafasi ya ulinzi kwa muda.

XS
SM
MD
LG