Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:21

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali yamaliza rasmi kazi za kulinda nchini humo


Wanachama wa kikosi cha MINUSMA Guinea wakivuta gari lao la kusindikiza lililokwama wakati wa msafara wa vifaa kutoka Gao hadi Kidal.Februari 2017.REUTERS
Wanachama wa kikosi cha MINUSMA Guinea wakivuta gari lao la kusindikiza lililokwama wakati wa msafara wa vifaa kutoka Gao hadi Kidal.Februari 2017.REUTERS

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali ilimaliza rasmi kazi za kulinda amani ya miaka 10 nchini humo siku ya Jumatatu, msemaji wake alisema, katika amri ya kuondoka iliyotolewa na viongozi wa kijeshi wa Mali.

Fatoumata Kaba Msemaji wa ofisi inayojulikana kama MINUSMA, alisema bendera ya Umoja wa Mataifa ilishushwa kwenye makao yake makuu katika mji mkuu Bamako.

Kaba alisema sherehe hiyo inaashiria mwisho rasmi wa kazi hiyo ingawa baadhi ya vipengele vyake bado vipo. Awamu ya kumalizia itakamilika baada ya tarehe ya mwisho ya kutakiwa kuondoka ya Januari mosi inayohusisha shughuli kama vile kukabidhi vifaa vilivyobaki kwa maafisa wa serikali.

Utawala wa kijeshi wa Mali, ambao ulichukua Madaraka mwaka 2020, mwezi Juni uliamuru kuondoka kwa ofisi hiyo licha ya kuwa katika hali ngumu ya ghasia za weapiganaji wa itikadi kali za kislamu na migogoro mingine.

Kuondoka kwa jeshi la Umoja wa Mataifa la kuleta utulivu liliokuwepo tangu mwaka 2013, kumezusha hofu kwamba mapigano yataongezeka kati ya wanajeshi na makundi yenye silaha kwa ajili ya udhibiti wa maeneo.

MINUSMA kwa muongo mmoja uliopita imedumisha takriban wanajeshi 15,000 na polisi nchini Mali.

Takriban wanajeshi 180 wameuawa katika mazingira ya uhasama, wengi wao wakilaumiwa kutokana na makundi yenye silaha yanayohusishwa na Al-Qaeda au kundi la Islamic state.

Hadi kufikia Ijumaa, zaidi ya wanajeshi na wafanyakazi raia 10,500 wa MINUSMA walikuwa wameondoka nchini Mali, kati ya takriban 13,800 waliokuwepo mwanzoni mwa kuondoka huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema kwenye X.

Tangu kuambiwa iendoke, MINUSMA hadi sasa imeacha nyadhifa 13 nchini Mali, lakini bado haijaondoka katika maeneo ya Gao na Timbuktu kaskazini.

Wiki iliyopita, ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikabidhi kambi ya Mopti katikati mwa Mali, moja ya maeneo yanayokumbwa na ghasia za wanajihadi ambazo zimekumba eneo la Sahel katika miaka ya karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG