Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 22:24

Marekani itaendelea kuwasaka magaidi - Obama


President Barack Obama spoke about the mass shooting earlier this week in San Bernardino, California, during his weekly Saturday address, Dec. 5, 2015.
President Barack Obama spoke about the mass shooting earlier this week in San Bernardino, California, during his weekly Saturday address, Dec. 5, 2015.

Rais Barack Obama alitumia hotuba ya nadra kutoka ofisi ya yake ndani ya White House Jumapili usiku kuzungumzia sera za serikali yake katika kupambana na ugaidi duniani hasa kundi la ISIL au Islamic State.

Akilihutubia taifa kufuatia shambulizi ambalo liliuwa watu 14 na kujeruhi wengine 20 katika mji wa San Bernadino, California wiki iliyopita Rais Obama kwa mara ya kwanza alitamka kuwa shambulizi hili linachunguzwa kama shambulizi la kigaidi.

Katika kueleza sera ya serikali yake dhidi ya ugaidi Rais Obama alisema Marekani haitaogopa kupambana na ugaidi kwa sababu "uhuru una nguvu kuliko hofu."

Baadhi ya mada kuu katika hotuba yake ni:

  • Marekani itaendelea kuwasaka na kuliangamiza kundi la ISIL na magaidi wengine
  • Marekani itashirikiana na mataifa marafiki duniani katika kupambana na ugaidi
  • Marekani itafanya hivyo bila kuweka kando thamini na tamaduni za taifa hili
  • Marekani itaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa usalama Syria na Iraq kupambana na ugaidi.
  • Marekani itashirikiana na nchi zenye waislamu wengi na jumuiya za kiislamu ndani ya Marekani kupambana na watu wachache wanaopindisha thamini za kiislamu

Rais Obama pia aliorodhesha mambo ambayo Marekani haitafanya katika mapambano na ugaidi.

  • Marekani haitajiingiza katika vita virefu kama vile vya Iraq "kwa sababu hicho ndio ISIL inachotaka
  • Wamarekani wasigeukiane wenyewe kwa wenyewe kwa kufanya vita hivi ni vita vya Amerika dhidi ya uislamu
  • Ni jukumu pia la viongozi wa kiislamu duniani na ndani ya Marekani kukiri kuwa itikadi za kigaidi ni hatari katika imani na lazima zishirikiane kuhakikisha zinashindwa.

Obama alisema viongozi wa kiislamu ni vyema washirikiane na marekani ili kupinga itikadi za chuki ambazo Al-qaida na IS wanazihamasisha. Pia alisema ni jukumu la wote wamarekani wa kila dini kupinga dhana kwamba wamarekani waislamu lazima watendewe tofuati na wengine. Amesema hiyo itakuwa ni sawa na kukubaliana na IS.

Katika kuorodhesha hatua ambazo serikali yake inachukua Obama alisema ameiamuru wizara ya mambo ya nje na usalama wa ndani kutathmini mpango wake maalum wa utoaji wa visa kama ulivyotumiwa na mwanamke aliyehusika katika shambulizi la California. Amelitaka bunge kuhakikisha hakuna mtu ambaye yuko kwenye orodha ya washukiwa kuwa na uwezo wa kununua silaha. Amesema ni vyema tufanye iwe vigumu sana kwa watu kununua silaha ambazo zinatumika kwa mashambulizi.

XS
SM
MD
LG