Baada ya zaidi ya wiki moja ya mapambano ya kijeshi kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini Rais Obama alitoa ujumbe wa Video kwa wananchi na serikali za Sudan na sudan kusini.
Katika ujumbe wake ulochapishwa siku ya ijuma kwenye tovuti ya Youtube, kiongozi wa marekani alisema, "haija bidi kufuata njia hiyo. Ugomvi unaweza kuepukwa," alisema. "Mungali muna nafasi ya kujiepusha kutumbukia tena katika vita, ambavyo vitaelekea njia moja tu, maafa zaid, wakimbizi zaidi vifo zaidi, kutoweka ndoto zenu na za watoto wenu"
Obama amesema hakuna suluhiso la kijeshi kwa ugomvi wowote. Alitoa wito kwa marais wa nchi hizo mbili kuonesha ushujao wao na kurudi kwenye meza ya mazungumzo.
"Ni lazima kwa serikali ya Sudan kusitisha hatua zake zote za kijeshi ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya anga. Ni lazima iwapatiye wafanyakazi wa huduma za dharura nafasi kuingia kuokoa maisha ya wanaohitaji msaada." Aliendelea kusima, " Kwa upande mwengine, ni lazima kwa serikali ya Sudan Kusini kukomesha uungaji mkono wa makundi yenye silaha ndani ya Sudan, na ni lazima isitishe hatua za kijeshi za kuvuka mpaka."