Ni mabadiliko ya nadra kutokana na upinzani uliopo juu ya udhibiti wowote mpya kwa bunduki kwa taasisi hiyo ya upinzani (NRA) yenye nguvu na yenye kupinga hatua zozote mpya za kudhibiti bunduki.
Kifaa cha Bump Stocks kama kinavyojulikana kilikuwa kikifahamika kidogo juu ya namna kinavyofanya kazi kwenye silaha hadi wiki hii ambapo mtu mwenye silaha aliuwauwa watu 58 na kuwajeruhi mamia huko Las Vegas alipotumia kifaa hicho kwenye silaha 12 zilizokutwa ndani ya chumba chake hotelini.
Rais Donald Trump alipoulizwa juu ya kifaa hicho wakati alipoanza mkutano na viongozi wa jeshi la Marekani Alhamis jioni alisema kwamba tutaliangalia hilo katika muda mfupi ujao. Chama cha National Rifle Association-NRA ambacho kinapinga vikali mapendekezo ya udhibiti wa bunduki hivi sasa kinasema kinapendelea ifanyike tathmini juu ya uhalali wa Bumb Stocks kifaa kinachowezesha risasi kujisukuma haraka zaidi katika silaha bila kutumia kifaa kingine kila wakati risasi inapofyatuliwa.