Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:16

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki ghafla akiwa na umri wa miaka 56


Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Serikali ya Burundi inasema Rais Pierre Nkurunziza amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 56.

Serikali imetoa taarifa katika mtandao wa twitter ikisema Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo Jumatatu katika hospitali ya Karusi mashariki mwa Burundi.

Nkurunzinza aliripotiwa kuwa katika hali mahtuti Jumatatu, na Idhaa ya Kinyarwanda ya Sauti ya Amerika iliripoti ongezeko la wanajeshi kuzungukia maeneo ya hospitali hiyo.

Taarifa iliyosomwa na msemaji wa Serekali Prosper Ntahorwamiye kupitia radio na televisheni ya taifa, imesema Nkurunzinza alianza kuugua usiku wa Jumamosi kuamkia jumapili, na kupelekwa katika hospitali ya Karusi kupata matibabu.

Jumamosi, alikua katika mkoa wake wa kuzaliwa wa Ngozi, akitizama mchezo wa Volleyball, Lakini mchana wa tarehe 8 juni, hali yake ilizidi kuwa mbaya akisikia kubanwa moyo, ameeleza msemaji wa serekali Prosper Ntahorwamiye, akiongeza kuwa ma daktari walijitahidi kumponya bila maafanikio.

Wiki mbili zilizopita mke wa Nkurunziza, Denise, alikimbizwa Nairobi, Kenya na ripoti zilisema kuwa alikuwa anaugua ugonjwa wa Covid-19.-Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington DC

Nkurunzinza amekuwa rais wa Burundi kwa awamu tatu. Uamuzi wake wa kugombania awamu ya tatu mwaka 2015 ulizusha mgogoro mkubwa nchini humo na kusababisha maelfu ya watu kukimbia nchi hiyo.

Alitazamiwa kuondoka madarakani mwezi August baada ya Jenerali Evariste Ndayishimiya kushinda uchaguzi mkuu mwanzoni mwa mwezi huu.

Kutokana na kifo hicho, serekali inatangaza msiba wa kitaifa wa siku 7 kuanzia leo tarehe 9 juni, na bendera zote zitapandishwa nusu mlingoti.

XS
SM
MD
LG