Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:20

Mkataba mpya wa matumizi ya mto Nile wasainiwa


Mto Nile ambao ni mkubwa kuliko yote duniani na nchi unazopitia.
Mto Nile ambao ni mkubwa kuliko yote duniani na nchi unazopitia.

Nchi ne za Afrika Mashariki na Kati zimetia saini mkataba mpya wa matumizi ya maji ya mto Nile, katika sherehe zilizofanyika huko Entebbe Uganda mwishoni mwa juma.

Nchi ne za Afrika Mashariki na Kati zimetia saini mkataba mpya wa matumizi ya maji ya mto Nile, katika sherehe zilizofanyika huko Entebbe Uganda mwishoni mwa juma.

Nchi hizo ni Tanzania, Uganda, Kenya Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Rwanda na Burundi.

Waziri wa maji na umwagiliaji wa Tanzania Profesa Mark Mwandosya ameiambia Sauti ya Amerika kuwa mkataba huo utaziwezesha nchi hizo kutumia maji ya mto huo katika shughuli mbalimbali kama vile kilimo na umwagiliaji.

Amesema idadi ya watu katika nchi hizo imeongezeka na haiwezekana mkataba uliotiwa saini mwaka 1929 wakati wa ukoloni unaozipa fursa Misri na Sudan kutumia maji ya mto huo kwa kiwango kikubwa ukaendelea wakati nchi hizo saba ambako ndiko chanzo cha mto huo ziendelea kutunza vyanzo vya mto huo bila kutumia maji.

Mwandosya amesema Sudan na Misri ambazo ndio watumiaji wakubwa wa maji ya mto nile wameshiriki katika majadiliano ya mkataba huo mpya kwa miaka kumi na mitatu lakini hawajakubaliana na vipengele vyote kumi na vitano vilivyomo katika mkataba huo.

Misri na Sudan zimekuwa ndio nchi zinazotumia maji ya mto Nile kwa kiwango kikubwa kufuatia mkataba wa mwaka 1929 uliotiwa saini na Waingereza.

XS
SM
MD
LG