Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 18:05

Niko tayari kuzungumza na vijana wanaogoma-Ruto asema


Vijana wakiwa kwenye mgomo mjini Nairobi. June 18 2024.
Vijana wakiwa kwenye mgomo mjini Nairobi. June 18 2024.

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo na maelfu ya vijana waliofanya maandamano kote nchini wiki hii ya kupinga kupitishwa kwa mswada ambao ungepelekea kuongezwa kwa ushuru, afisa kutoka ofisi ya rais amesema  Jumapili.

Maandamano hayo, ambayo yamekuwa yakiongozwa na kizazi maarufu kama Gen-Z, wakati yakirushwa moja kwa moja kwenye majukwaa ya kimitandao, hayakutarajiwa na serikali, huku taharuki kuhusu sera za kiuchumi za Ruto ikiongezeka. “Vijana wetu wamejitokeza na kuangazia masuala yanayohusu taifa lao. Wametekeleza jukumu lao la kidemokrasia na ni hatua ya kujivunia,” amesema Ruto kulingana na msemaji wa ofisi ya Rais Hussein Mohamed kupitia ukurasa wa X.

Tayari watu wawili wamekufa huku wengine wengi wakijeruhiwa wakati wa maandamano hayo kwenye mji mkuu wa Nairobi, kwa mujibu wa watetezi wa haki. Maandamano hayo yalianza Nairobi Jumanne, kabla ya kuenea kwenye miji mingine kote nchini, wakati waandamanji wakiitisha maandamano ya kitaifa Jumanne Juni 25. Utawala wa Ruto umetetea hatua ya kuongeza ushuru, ukidai kuwa itaongeza kipato cha serikali, pamoja na kuzuia utegemezi wa mikopo kutoka nje.

Forum

XS
SM
MD
LG