Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:07

Nikki Haley atangaza kugombea urais wa Marekani


Gavana wa zamani wa South Carolina, Nikki Haley, Jumanne amesema kwamba atagombania uteuzi wa mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Republikan.

Hii inamfanya Haley kukabiliana na bosi wake wa zamani rais Donald Trump, ambaye alimteua kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Haley mwenye umri wa miaka 51, alitangaza kupitia mitandao ya kijamii akisema rekodi ya rais Joe Biden hairidhishi, na ni wasaa wa kiongozi wa kizazi kipya.

Katika video hiyo ya zaidi ya dakika tatu, haikumtaja kabisa rais mstaafu Trump, ambaye mwezi Novemba alitangaza kuwa pia atawania uteuzi wa chama cha Republikan kugombea tena urais ambao alishindwa na rais Joe Biden katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Katika video hiyo ameelezea miaka ya mwanzo akiwa South Carolina kama binti wa muhamiaji muhindi, ambaye alifanikiwa kuwa gavana kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017 na kupewa wadhifa wa ubalozi wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 mpaka 2018.

XS
SM
MD
LG