Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:00

Rais wa Nigeria Yar'Adua afariki dunia


Rais Umaru Yar'Adua
Rais Umaru Yar'Adua

Serikali ya Nigeria ilitangaza Jumatano usiku kwamba rais Umaru Yar’Adua amefariki baada ya ugonjwa wa muda mrefu. Tangazo kwenye redio ya taifa lilieleza kwamba Bw Yar’Adua alifariki usiku wa jumatano katika makazi ya rais akiwa na umri wa miaka 58

Msemaji wa Rais Olusegun adeniyi amesema Rais Yar'adua alifariki majira ya saa tatu usiku huko Nigeria. Televisheni ya taifa ilisitisha matangazo yake ya kawaida kwa kutoa tangazo lifuatayo:

“Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Al-hajji Musa Yar’Adua amefariki saa machache iliyopIta katika makazi ya rais. Washauri wa usalama walimuarifu mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Jenerali Aliyu Gusau. Gusau mara moja alimuarifu Kaimu Rais. Marehemu Rais alikua anauguwa kwa muda mrefu".

Tangazo hilo halikutoa sababu rasmi ya kifo. Rais Yar’Adua alikua anugua ugonjwa wa figo kwa muda mrefu lakini alilazwa katika hospitali huko Saudi Arabia kwa miezi kadhaa kwa matibabu ya moyo kabla ya kurudi Nigeria miezi miwili iliyopita.

Alipokua nje ya nchi wabunge wa Nigeria walimpatia makamu wake Goodluck Jonathan madaraka ya kua Kaimu Rais. Na tangu wakati huo Jonathan amefanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri na kueleza kwamba utawala mpya utachukua hatua za kishuja kuimarisha miundo mbinu ya nchi kuongeza huduma ya umeme na kuendelea na juhudi za kuleta utulivu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

Kifo chake kinaacha mgawanyiko katika chama tawala. Kaimu Rais hajaweka kando uwezekano wa kugombania kiti cha urais hapo mwakani. Lakini yeye anatoka kusini mwa Nigeria na Rais wa chama tawala anasema mgombea mpya wa chama ni lazima atoke kaskazini.

XS
SM
MD
LG