Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Nigeria yatishia kuichukulia hatua kali BBC kwa kupeperusha filamu kuhusu magenge ya uhalifu


Nembo ya BBC kwenye makao makuu ya shirika hilo la utangazaji mjini London.
Nembo ya BBC kwenye makao makuu ya shirika hilo la utangazaji mjini London.

Serikali ya Nigeria Alhamisi imetishia kuliwekea vikwazo shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) na shirika lingine la habari nchini humo kwa “kutukuza ugaidi” baada ya kuonyesha filamu kuhusu wababe wa kivita wa magenge ya uhalifu kaskazini magharibi mwa nchi hiyo

Eneo la vijijini la kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanakabiliwa na mauaji yanayofanywa na magenge yenye silaha nzito yanayojulikana ndani ya nchi kama majambazi ambao wanavamia vijiji kwa kupora na kuteka nyara wakazi wengi kwa ajili ya kupewa fidia.

BBC Africa eye katika filamu yake iitwayo “Majambazi wababe wa kivita wa Zamfara” iliwahoji wanachama wa magenge hayo na waathiriwa ili kuchunguza machafuko katika jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara.

Kituo cha televisheni, Trust TV, ambacho ni sehemu ya shirika la habari la ndani Daily Trust media, pia kilipeperusha mahojiano na kiongozi mashuhuri wa majambazi katika filamu hiyo kuhusu machafuko hayo.

Waziri wa habari Mohammed Lai amewambia waandishi wa habari kwamba tume ya kitaifa ya utangazaji inachunguza iwapo vyombo hivyo viwili vya habari vilikiuka kanuni za utangazaji.

“Naweza kuwahakikishia, kutakuwa na madhara”, waziri huyo amesema.

“Hawatakwepa hatua na utukuzaji huu wa wazi wa ugaidi na ujambazi nchini Nigeria,” ameongeza.

BBC katika taarifa yake jana Alhamisi, imesema inatetea ripoti hiyo.

“BBC Africa Eye mara nyingi inajihusisha na masuala yenye utata na magumu,” imesema.

“Hadithi hii ni kwa manufaa ya umma na BBC inatetea uandishi wake wa habari,” taarifa hiyo imeongeza.

XS
SM
MD
LG