Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kwamba huduma hiyo itarejeshwa leo Alhamisi kulingana na mratibu mkuu wa kitaifa wa maendeleo ya habari na teknolojia Kashifu Inuwa Abdullahi.
Abdullahi ameongeza kusema kwamba hatua hiyo imechukiliwa baada ya Twitter kukubali baadhi ya masharti yaliowekwa na serikali ya Nigeria. Twitter ilipigwa marufuku kutokana na madai ya serikali kwamba ilikuwa ikitumika kwa shughuli ambazo zingehujumu utaifa wa Nigeria.
Hatua hiyo hata hivyo ilikosolewa pakubwa kutokana na kuwa ilichukuliwa muda mfupi baada ya ujumbe wa rais akionya waasi kwamba angewashugulikia kwa lugha ambayo wangeelewa kuondolewa na kampuni hiyo.
Abdullahi ametetea hatua hiyo akisema ilikuwa muhimu katika kutadhmini tena uhusiano wao na kampuni ya Twitter. Kupitia taarifa amesema kwamba uhusiano wa Twitter na serikali yake umekuwa wenye heshima na maelewano.