Vyombo kadhaa vya habari vya Nigeria vimesema watu hao wenye silaha walifyatulia risasi waumini na kulipua mabomu kwenye kanisa la mtakatifu Francis katika mji wa Owo. Washambuliaji hawakutambulika na nia yao haikufahamika mara moja.
“Inasikitisha sana kwamba wakati misa takatifu ikiendelea, watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia kanisa la mtakatifu Francis, watu wengi wanaohofiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa na kanisa kuvamiwa,” alisema msemaji wa kanisa katoliki nchini Nigeria, mchungaji Augustine Ikwu.