Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:08

Nigeria: Watu 15 wafariki katika ajali ya boti


Ramani ya Lagos, Nigeria
Ramani ya Lagos, Nigeria

Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti katika mji wa biashara wa Nigeria Lagos imeongezeka na kufikia 15 huku miili zaidi ikiopolewa, maafisa wa dharura wamesema Jumapili.

“Kulikuwa abiria 16 ndani ya boti wakati ajali ilipotokea Ijumaa usiku,” Ibrahim Farinloye wa idara ya kitaifa ya dharura (NEMA) ameiambia AFP.

Maiti mbili zilipatikana baada ya mkasa huo Jumamosi, amesema.

Amesema miili 11 iliopolewa Jana Jumapili.

“Kujumuisha na hiyo, jumla ya miili 15 imeopolewa.”

Farinloye amesema abiria mmoja ametoweka.

Mamlaka ya Lagos ya usafiri wa baharini (LASWA) pia imethibitisha vifo hivyo.

XS
SM
MD
LG