Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:40

Nigeria: Wanafunzi Waislamu wamuua kwa mawe mwanafunzi Mkristo wakimtuhumu kumkashifu Mtume Muhammad


Ramani ya Nigeria
Ramani ya Nigeria

Wanafunzi Waislamu katika mji wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Sokoto Alhamisi wamempiga mawe mwanafunzi Mkristo hadi kufa na kuchoma maiti yake baada ya kumshtumu mwanafunzi huyo wa kike kwamba alimkashifu Mtume Muhammad, polisi wamesema.

Darzeni ya wanafunzi wa chuo cha elimu cha Shehu Shagari walifanya vurugu baada ya mwanafunzi mwenzao Deborah Samuel kutoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo waliiona kuwa inamvunjia heshima Mtume Muhammad, msemaji wa polisi huko Sokoto Sanusi Abubakar amesema katika taarifa.

Wanafunzi walimuondoa kwa nguvu muathirika kwenye chumba cha usalama ambako alikuwa amefichwa na viongozi wa shule, wakamua na kuchoma jengo hilo, Abubakar amesema.

Abubakar amesema washukiwa wawili walikamatwa kufuatia tukio hilo.

Sokoto ni miongoni mwa darzeni ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria ambako sheria kali ya Kiislamu au Sharia inatekelezwa.

XS
SM
MD
LG