Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:50

Nigeria: Waandamanaji washambulia mashine za benki kutokana na uhaba wa pesa taslimu


Watu wakipiga foleni kuchukua noti mpya za naira kwenye mashine moja ya Benki huko Maiduguri, Januari 29, 2023. Picha ya AFP
Watu wakipiga foleni kuchukua noti mpya za naira kwenye mashine moja ya Benki huko Maiduguri, Januari 29, 2023. Picha ya AFP

Wafanya vurugu Jumatano walishambulia mashine za Benki za ATM na kuziba barabara katika miji mitatu ya Nigeria huku hasira zikiongezeka mitaani kutokana na uhaba wa pesa taslimu, maafisa na vyombo vya habari vya nchini vimesema.

Nigeria imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa pesa taslimu tangu Benki Kuu ilipoanza kubadilisha noti za zamani za sarafu ya naira na noti mpya, na kusababisha upungufu wa noti.

Mabenki yalipunguza upatikanaji wa pesa taslimu na kuchukua pesa kwenye mashine za ATM kwa sababu ya uhaba wa noti mpya, na baadhi ya wafanyabiashara wanakataa kupokea noti za zamani za naira, na kusababisha foleni kubwa, kuwakasirisha wateja na kuvuruga biashara.

Ghasia katika mji wa kusini magharibi wa Ibadan, mji wa Benin na jimbo la kusini la Delta zinajiri kabla ya Nigeria kufanya uchaguzi tarehe 25 Februari kuamua juu ya mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye anaondoka madarakani baada ya mihula miwili.

Polisi katika jimbo la Delta wamesema vijana waporaji kwa kujificha nyuma ya maandamano walichoma benki mbili na magari mawili.

Msemaji wa polisi wa jimbo Bright Edafe aliandika kwenye Twitter “Tumewakamata washukiwa tisa kufikia sasa. Baadhi ya watu wataendelea kudai kuwa haya ni maandamano.”

XS
SM
MD
LG