Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 10:38

Nigeria: Ukosefu wa usalama waweza kupelekea kuahirishwa kwa uchaguzi wa Februari-Tume ya uchaguzi


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akizungumza wakati wa uzinduzi wa sarafu mpya ya Nigeria mjini Abuja, Novemba 23, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akizungumza wakati wa uzinduzi wa sarafu mpya ya Nigeria mjini Abuja, Novemba 23, 2022. Picha ya Reuters

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria Jumatatu imesema uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwezi Februari unaweza kufutwa au kuahirishwa ikiwa ukosefu wa usalama hautashughulikiwa.

Rais Muhammadu Buhari ambaye ataachia ngazi baada ya kuhudumu mihula miwili anaondoka madarakani bila kumaliza uasi wa miaka 13 wa wanamgambo wa Kiislamu eneo la kaskazini mashariki, huku kukiwa ongezeko la uhalifu mbaya kaskazini magharibi na katika majimbo ya katikati mwa nchi vile vile mivutano ya kujitenga kusini mashariki.

“Ikiwa ukosefu wa usalama hautafuatiliwa na kushughulikiwa kwa uthabiti, mwishowe unaweza kupelekea kufutwa au kuahirishwa kwa uchaguzi katika maeneo bunge mengi na kudhoofisha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi,” amesema Abdullahi Abdu Zuru, mwenyekiti wa tume huru ya kitaifa ya uchaguzi.

Amesema hali hiyo “inaweza kuchochea mzozo wa kikatiba, na kuongeza kuwa lazima hali hiyo isiruhusiwe kutokea na haipaswi kuruhusiwa kutokea”.

XS
SM
MD
LG