Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:58

Nigeria kuwaadhibu waliohusika na shambulizi kwa raia


Serikali ya Nigeria, Alhamisi iliahidi kuwaadhibu waliohusika na shambulizi la ndege zisizo na rubani na kuua takriban raia 85 kimakosa huku shutuma na wito wa kufanyika uchunguzi ukiongezeka.

Jeshi limesema wanajeshi walikuwa wakifanya doria za anga Jumapili walipoona kundi la watu kaskazini magharibi mwa Jimbo la Kaduna, na kutafsiri vibaya mtindo wao wa shughuli kuwa sawa na wa wanamgambo.

Ndege isiyo na rubani ilishambulia kijiji cha Tudun Biri, kimakosa wakati wakazi walipokuwa kwenye sherehe. Vyanzo rasmi vimesema takriban watu 85 waliuwawa na wengine 66 kujeruhiwa.

Vikosi vya jeshi la Nigeria, mara nyingi hutegemea mashambulizi ya anga katika vita vyao dhidi ya wanamgambo kaskazini magharibi na kaskazini mashariki mwa nchi, ambapo wanamgambo wenye msimamo mkali wamekuwa wakipigana kwa zaidi ya muongo mmoja.

Forum

XS
SM
MD
LG