Polisi wamesema kwamba watu hao walikishambulia kituo cha gari moshi katika mji wa Igueben, jimbo la Edo na kutwaeka nyara watu kadhaa waliokuwa wanasubiri kusafiri.
Msemaji wa polisi katika jimbo la Edo Chidi Nwabuzor, amesema kwamba watu hao walifyatua risasi kadhaa hewani kabla ya kuwateka abiria.
Baadhi ya abiria walijeruhiwa, na polisi wamesema kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.
Watu saba waliuwawa na wengine kadhaa kutekwa nyara mwaka uliopita katika shambulizi dhidi ya kituo cha treni karibu na mji mkuu wa Abuja.