Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 02, 2024 Local time: 21:06

Niger yataka idara za upelelezi kuwasaka awfungwa walio toroka


Wizara ya mambo ya ndani ya Niger, imesema imeagiza vitengo vya upelelezi kuwa macho baada ya wafungwa kutoroka Alhamisi katika gereza lenye ulinzi mkali la Koutoukale ambalo wafungwa wake ni pamoja na wanamgambo wenye msimamo mkali.

Taarifa ya wizara haikusema idadi ya wafungwa waliotoroka Koutoukale, iliyopo kilomita 50 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Niamey, au jinsi walivyofanikisha kutoroka. Mwaka 2016 na 2019, jaribio la wafungwa kutoroka lilizimwa.

Wafungwa wa gereza hilo ni pamoja na wale kutoka katika mzozo wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi na makundi yenye silaha yanayohusishwa na al Qaeda, Islamic State na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Boko Haram.

Mamlaka za eneo hilo zimeweka amri ya kutotoka nje usiku kucha katika wilaya ya mjini ya Tillaberi, ambayo iko katika eneo moja na gereza lakini haikutoa maelezo zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG