“Jeshi litarejea kwenye mapigano makali hadi Hamas itakaposhindwa,” Netanyahu alisema katika taarifa ya video Jumanne.
Rais wa Marekani Donald Trump awali alipendekeza kufutwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas ikiwa mateka wote hawataachiliwa ifikapo Jumamosi.
Trump alitoa matamshi hayo Jumatatu baada ya Hamas kuishtumu Israel kukiuka sitisho la mapigano na kutishia kuchelewesha mpango wa kuwaachilia mateka watatu wanaotarajiwa kuachiwa huru Jumamosi.
Afisa wa Hamas alisema Jumanne kwamba njia pekee kwa mateka kuachiliwa ni kuheshimu masharti ya makubaliano.
Forum